Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania siku ya leo amemjibu maombi ya moja kwa moja juu ya kilio cha wasanii kilichowakilishwa na msanii Diamond Platnumz.
Akizungumza moja kwa moja kutoka Ikulu Rais Magufuli kupitia Simu aliyoipiga kipindi cha Clouds 360, Rais alimueleza Diamond kuwa maombi yake ameyasikia na atayafanyia kazi kwa ukaribu.
Aidha Rais Magufuli amempongeza Diamond kwa moyo wake wa kujituma na kazi nzuri anazofanya kwa jamii pia amefurahishwa na msanii huyo kupata watoto wawili kwasasa kwani kipindi cha kampeni alikuwa na mtoto mmoja
kilichomeweka gumzo ni pale Rais Magufuli alipogusia kuwa anavutiwa pia na kipindi cha SHILAWADU Rais alisema kuwa anavutiwa sana na jinsi wanavyoigiza kipindi chao.
0 Comments