Mkali kutoka WCB, Harmonize ameachia kazi mpya tatu kwa wakati mmoja, Happy Birthday, Acha Nilewe na Niambie.
Kati ya hizo, Happy Birthday inapatikana mtandaoni kwa njia ya kawaidanna Acha Nilewe pamoja na Niambie zinapatikana Wasafi.com japo Niambie ndio Ngoma ambayo Jumatano hii inatambulishwa rasmi redioni.
Kitendo hicho kimemkwaza Producer Fraga kutoka Uprise Music ambaye ametengeneza Acha Nilewe na Happy Birthday kwakuwa alitegemea ngoma hizo mbili zingetolewa kwa mfumo rasmi,na sio kuwekwa tu mtandaoni.
“Haiwezekani ukaachia nyimbo tatu kwa wakati mmoja, halafu zile nilizozifanya mimi kama dizaini fulani kazitupa mtandaoni halafu kuna moja kaiachia official. Kwahiyo kitu kile mimi zijapendezewa nacho kwa sababu naona kama amedharau kazi zangu. Kwanini asingesubiri wakati ungefika angeachia kwa utaratibu ambao ni mzuri,” amelalamika Fraga kupitia kipindi cha Supermega cha Kings Fm kinachoongozwa na Prince Ramalove.
Pia Producer huyo amedai kuwa kwa nyimbo zote ambazo amemtengenezea Harmonize, Bado, Acha Nilewe na Happy Birthday hakuna hata nyimbo moja ambayo amewahi kumtoza msanii huyo kwani aliamini zikitoka atapata kazi zingine nyingi kupitia Harmonize.
Awali Fraga aliitumia ujumbe Bongo5:
Ngoma hizi mbili nilizo produce mimi ameamua kuziachia mtandaoni naweza sema amezitupa, kitendo hicho sijakipenda kwasababu naona amenidharau,amedharau jitihada na juhudi nilizotumia kufanya hizo kazi. Ukizingatia Harmonize ni mshikaji wangu hivyo sikuwa mchaji gharama yoyote kwaajili ya kazi zake!Kwa matarajio kwamba kazi zikitoka,nitapata kazi zingine za kuniingizia pesa kutoka kwa wasanii wengine!! Sasa leo kazi zote nilizofanya mimi amezitupa tu mtandaoni! Kana kwamba ni uchafu fulani hivi. Ngoma ya kwanza kumfanyia Harmonize ilikuwa Acha Nilewe mwezi wa 12 mwaka 2015, hapo hapo tukatengeneza Bado aliyomshirikisha Diamond kwa kipindi hicho wakaamua kutoa Bado.Baadaye tukatengeneza “Happy Birthday mwaka jana cha ajabu nguvu na jitihada nilizotumia kufanya kazi za huyu Harmonize zinaishia kutupwa!! Kiukweli imenivunja moyo! Mbaya zaidi ni pale nilipo jaribu kumtumia ujumbe yaani sms kuuliza kwanini hizi ngoma umeamua kuzitupa mtandaoni? Hakunijibu chochote japo sms alizisoma.. Mimi naona kuwa amenidharau
0 Comments