Muigizaji wa filamu nchini Tanzania Gabo Zigamba amewataka waongozaji filamu Tanzania (Directors) kutojihusisha na kazi za kuongoza filamu kama hawana vipaji pamoja na taaluma hiyo.
Gabo amesema watu hao ndiyo wanasababisha soko la filamu nchini kupigwa bao na kazi kutoka nje kwa maana kazi wanazozitengeneza kukosa ubunifu na ushindani kama ilivyokuwa zamani kupelekea watazamaji kuichukia 'Bongo Movie'.
"Kuwa 'director' siyo suala la kukurupuka tu, si maamuzi ya kufikirika tu ukaamua kufanya hivyo lakini kila kinachofanyika lazima kiwe kina taaluma ila nasisitiza na kuwaambia watu wasifanye vitu bila ya kuwa na taaluma navyo, ukifanya kitu chenye taaluma nacho itakuwa kwenye ubora".Alisema Gabo
Aidha msanii huyo amesema kwa upande wake watu wasahau kwa sasa kwa yeye kuwa muongozaji filamu na kama atataka kufanya hivyo basi atafanya kwa utaalamu na siyo kukurupuka.
0 Comments