MICHAEL MTANZANIA

ONESTEPMEDIATZ

Hili ndilo swali ambalo Mr T Touch hawezi kulijibu kuhusu Nay wa Mitego

Ni muda sasa tangu Producer Mr T Touch aondoke Free Nation inayomilikiwa na Nay wa Mitego na kwenda kuanzisha studio yake mitaa ya Sinza Palestina jijini Dar es Salaam.


Mbali na kwamba wawili hao walivunja biashara kwa kukosa maelewano,wengi tunaamini kuwa huenda siku moja wakakaa studio tena na kutengeneza ngoma kwa mara nyingine tena.

Kupitia Supermega ya Kings FM,Prince Ramalove alimuuliza Mr T Touch kama yupo tayari kufanya kazi tena na Nay wa Mitego, swali ambalo limeshindwa kujibiwa na producer huyo.

“Hilo swali silitaki,sababu sikutaka kulizungumzia kwenye mambo yangu,” amejibu kifupi Mr T Touch. Mbali na kulikwepa swali hilo,amemshauri producer mpya wa Free Nation,Ossam kuwa afanye juhudi zaidi na atafika anapopahitaji,kwani hata yeye mwanzo alikuwa na ndoto,akakaza na hatimaye amezifikia

Post a Comment

0 Comments