Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na EATV kupita twitter, zinadai kuwa baada ya Harmonize kumuona meneja wa Harmorapa, msanii huyo amemuoneshea kidole cha kati ambacho hudaiwa kuwa ni ishara ya tusi kisha akaondoka maeneo ya studio hizo.
“Tunaomba radhi kwa ishara aliyoionesha hapa na Hamorappa wakati akielezea kitendo kilichofanywa na Harmonize,” walitweet EATV.
Harmorapa akiongea katika kipindi hicho, amelaani kitendo hicho cha udharirishaji na kudai kuwa Harmonize amemtukana bosi wake kwa kumuonyesha ishara ya kidole cha kati baada ya kukutana.
“Kwa kweli sijapenda Harmonize amemtukana bosi wangu kwa kumuonesha kidole cha kati, sijapenda kabisa,” alisema Harmorapa.
Kwa upande wao, kituo cha EATV, kupitia Twitter kimeomba msamaha kwa watazamaji wake wote kutokana na kitendo hicho cha aibu kilichofanywa na msanii huyo.
0 Comments