CEO wa Wasafi, Diamond Platnumz amedai kuwa kitendo cha baadhi ya watangazaji na waandishi kushikilia kumzungumzia na kumuandika kwa Mambo mabaya, cha kujipotezea muda kwao
Kwenye exclusive interview na Prince Ramalove kupitia Kings FM, Diamond Alifafanua kauli yake ya kusema kuwa yeye hategemei Redio wala TV pindi anapotoa nyimbo zake kwa sasa.
“Unajua kwamba kuna kiwango unapofikia,unapokuwa na mashabiki wengi,lazima uongeze ufanisi wako wa usambazaji wa kazi zako.Tuna redio tuna TV, lakini pia lazima tuongeze namna zingine za kupromote kazi zako,” amesema Diamond.
“Wasanii wanatakiwa wajiongeze, sasa naona kuna watu wameichukua tofauti na kuipindua kumtengenezea mtu baya,lakini wanapoteza muda.”
Diamond ameongeza kuwa yeye anaheshimu vyombo vya habari na hata kama kuna watu wanadai amefika alipo kwa mchango wao, yeye anaheshimu pia.
0 Comments