Mahakama ya Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro imetoa hukumu ya
kuchwapwa kiboko kimoja mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya sekondari
Longoi wilaya hapo baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka na kumpa
ujauzito mwanafunzi mwenzake wa shule hiyo
Akisoma hukumu hiyo Hakimu mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Agnes
Muhina mbele ya mwendesha mashtaka wa polisi , Valeria Banda, alisema
kuwa anatoa hukumu hiyo baada ya kuridhishwa na ushaidi uliotolewa
mahakamani hapo usioacha shaka yoyote.
Kesi hiyo pia ilikuwa na mashahidi sita wa upande wa mashtaka akiwemo
daktari wa hospitali ya Hai,dawati la jinsia na watoto na mama mzazi wa
binti huyo, mwalimu na binti mwenyewe.
Ilidaiwa na mwendesha mashtaka wa polisi kuwa mtuhumiwa alitenda kosa
hilo Oktoba 10, 2015 saa 8.00 mchana katika kijiji cha Mkalama
Wilayani humo ambapo alimbaka na kumpa ujauzito mwanafunzi mwenzake wa
kidato cha tatu mwenye umri (16).
0 Comments