Mwanasiasa mmoja mwanamke anachukua hatua isio ya kawaida katika kile anachosema ni sheria kali za uavyaji mimba kwa kuwalenga wanaume wanaofanya punyeto.
Lengo la sheria hiyo yake anasema ni kuwalinda watoto ambao hawajazaliwa kila mahali
.
Ndio sababu anataka mwanamume atakayemwaga mbegu zake za kiume nje ya uke wa mwanamke ama kutengezwa nje ya kituo cha matibabu kutozwa faini ya dola 100.
Iwapo mwanamume atapatikana na hatia kwa kumwaga mbegu hizo nje itachukuliwa kama kitendo dhidi ya mtoto ambaye hajazaliwa.
''Iwapo inaonekana kama hatua isio ya kawaida basi hivyo ndivyo inavyopaswa kuwa''alisema Farrar.
Jessica Farrar , ni mwanachama wa Democrat katika bunge la wawakilishi jimbo la Texas aliyewasilisha muswada huo nambari 4260 wiki iliopita.
Anajua hautaidhinishwa kuwa sheria.
Lakin anasema kuwa sio rahisi zaidi ya kuwawekea wanawake sheria kali za uavyaji mimba katika jimbo la Texas wakati mtu anapochagua kutaka kuavya mimba.
Hatua yake ya mwisho ilikuwa hivi karibuni kuhusu miswada kadhaa ya wanawake anayosema inapunguza haki za wanawake.
Sheria ya hivi karibuni ilikuwa ile inayowashinikiza wanawake kuchagua kuzika ama kuchoma mabaki ya viinitete kutokana na mimba iliotoka ama ile iliotolewa.
Wakati wa kusikizwa kwa muswada huo mnamo mwezi Agosti, Seneta wa jimbo hilo Don Huffines alisema: kwa muda mrefu sasa Texas imeruhusu viumbe visivyo na hatia kutupwa na uchafu.
Iwapo tunachukulia hatua hizi na umuhimu mkubwa kwa sababu ya maisha ,basi, hatuwezi kupoteza hata mbegu moja.
lakini wakosoaji wake hawakupendelea .
''Huu ni ujinga wa wazi'' mtu mmoja alituma ujumbe wake katika mtandao wa Twitter akisema kuwa ''ni yai lililorutubishwa pekee ambalo linahitaji kulindwa akiuliza iwapo angeweza kutumia sheria hiyo dhidi ya wanawake walio katika hedhi.
Jimbo la Texas lina sheria kali za uvanyaji mimba nchini Marekani ijapokuwa mahakama ya juu ilibatilisha marufuku ya uavvaji mimba uliosababishwa na dawa baada ya wiki saba mwaka uliopita.
Sheria hiyo inamaanisha kwamba kliniki zinazoavya mimba ni chache mno.
Kulingana na gazeti la Tribune katika jimbo hilo kulikuwa na kiliniki 19 za uavyaji mimba mnamo mwezi Juni 2016, nyingi zikifanya kazi katika maeneo ya mijini.
0 Comments