Wakati wa vita ya pili ya dunia mwaka 1939 - 1945, huko Ujerumani chini ya utawala wa Adolf Hitler Wayahudi walikuwa wanauliwa kama kuku kutokana na chuki kubwa ya kiongozi huyo wa kinazi dhidi yao.
Kufuatia chuki hiyo kulitengenezwa kambi mbalimbali za mateso na mauwaji ya kinyama dhidi ya wayahudi, walikuwa wakikamatwa na kusafirishwa kwa treni mpaka ziliko kambi hizo na kisha kupata mateso na kuuwawa (tazama filamu ya Escape from Sobibor ya 1987).
Horst Petri alikuwa ni mmoja wa maofisa wa ngazi ya juu na wa karibu wa Hitler, hivyo kuwa ni mmoja wa watekelezaji wakubwa wa mateso na mauwaji dhidi ya wayahudi. Historia imeandika kuwa Wayahudi wana asili ya Israel, lakini kwasasa wanapatikana kote duniani.
Mwaka 1943 wakati maelfu ya wayahudi wakiwa njiani kupitia usafiri wa treni wakipelekwa katika moja ya kambi ya mateso, kuna wayahudi 6 walifanikiwa kutoroka na kujiokoa katika safari hiyo ya kifo, lakini kwa bahati mbaya wakakamatwa na Erna Petri ambaye ni mke wa Hosrt Petri.
Historia imeandika kuwa Erna aliwapatia huduma nzuri kwa karibia wiki zima, akiwapa mahala pazuri pa kulala pamoja na chakula kizuri, lakini baada ya siku hizo chache akawapeleka msituni ambako alikuwa ameandaa watu na wakawachinja kinyama.
Walikuwa na kauli mbiu yao iliyosema "Dunia bila wayahudi."
Baada ya vita na utawala wa Hitler kuisha, mwaka 1961 wote wawili mtu na mumewe wakakutwa na hatia ya kujibu juu ya mauwaji waliyoyafanya wakati huo, mahakama ikaamua mume ahukumiwe kifo na mke apewe kifungo cha maisha gerezani.
Horst Petri aliyebainika kuuwa zaidi ya raia 1,000 wa Kiyahudi alinyongwa December 22, 1962 huku mkewe Erna akihukumiwa jela maisha kwa kuuwa jumla ya Wayahudi 10, mpaka anafariki mwaka 2000 akiwa na miaka 80 bado alikuwa gerezani huko Hoheneck Germany.
0 Comments