Mwaka 1958 alichapisha kitabu kilichopata umaarufu mkubwa duniani kote kikitafsiriwa kwa lugha zaidi ya hamsini. Kitabu hiko kiliuza takribani nakala milioni 15 huku kikitumika kufundishia kwenye shule na vyuo mbalimbali ulimwenguni.
Mwaka 1966 alichapisha kitabu kingine ambacho kilitabiri matukio yaliyokuja kutokea siku za usoni. Katika kitabu hiko mwandishi alieleza kuhusu kupinduliwa kwa kiongozi mmoja aliyempa jina la 'Chifu Nanga' tukio ambalo lilikuja kutokea kweli kwani siku chache tu baada ya kuachiwa kitabu hicho nchini kwake kulifanyika mapinduzi yaliyopelekea kifo cha waziri mkuu wa nchi hiyo bwana Abubakar Balewa. Tukio hilo lilimfanya mwandishi aitwe 'nabii' kutokana na kuandika mambo yaliyokuja kuakisi uhalisia katika siku zilizofuata.
Alikuwa mwandishi mkubwa sana, aliyeheshimika ndani na nje ya mipaka ya nchi yake akifundisha katika vyuo mbalimbali nchini Nigeria na Marekani. Wengi walimuita 'Father of African Literature' yaani baba wa fasihi ya kiafrika.
Mwaka 1990 tukio la kusikitisha lilimfika. Akiwa mjini Lagos Nigeria alipata ajali ya gari iliyopelekea kupooza kwa mwili wake sehemu ya kiunoni kushuka chini. Hivyo tangu siku hiyo maisha yake yote yaliishia kwenye kiti cha magurudumu kama umuonavyo Pichani. Licha ya kuwa mlemavu, aliendelea kufundisha katika vyuo vikuu anuai huko nchini Marekani hadi pale mauti yalipomfika mwaka 2013.
0 Comments