11, 2017 mtandao wa The Sun wa Uingereza uliripoti taarifa ya wanandoa wawili waliowashangaza watazamaji wakiwa katika kipindi cha This Morning cha ITV ya Uingereza baada ya kudai kuwa mdoli wao mdogo unaoitwa Victoria ulimshambulia mmoja wao (mume) akiwa bafuni anaoga.
Wanandoa hao Debbie na Cameron Merrick wote wa umri wa miaka 50, walinunua midoli mitatu kutoka katika duka la mitumba kwa pauni 5 kama TZ14,000 hivi kila mmoja kwa matumaini kuwa wangeiuza kwa faida.
Wenzi hao walisimulia jinsi Cameron alivyohisi moto na kukwaruliwa na kucha za kiumbe mguuni wakati akiwa kuoga asubuhi baada ya kuuhamishia mdoli bafuni kwa sababu kilikuwa na marafiki waliwaotembelea nyumbani hapo.
Cameroon alisema: "Niliamka asubuhi na nilioga kama kawaida. Ghafoa niliangalia chini na kulikuwa na donda la kucha kwenye goti langu, sikujua limekujaje."
Walisisitiza kuwa hawakuwa na paka ndani labda aliingia kumkwarua Cameroon na haingekuwa Cameron mwenyewe ndiye amejikwarua kwani ana kucha fupi sana. Walieleza pia jinsi jana yake usiku walisikia kitu kinazunguka chini ya kitanda cha chumba chao cha kulala.
Haya yalikuwa ni mahojiano ya LIVE katika kipindi cha television cha This Morning cha ITV ya Uingereza mwaka huo 2017 lakini ajabu ni kuwa wakati wakiuelezea mdoli huo ambao walikua nao hapo studio pia, ulianza kuonekana ukichezesha kiti ulichokalia.
Taarifa za miezi kadhaa baadaye kutoka katika kipindi hicho zilisema kuwa mdoli huo ulikuwa umemshambuoia tena Cameroon wakati amelala usiku.
Mdoli aitwaye victoria akiwakweye kiti |
0 Comments