MICHAEL MTANZANIA

ONESTEPMEDIATZ

MFAHAMU BINADAMU MREFU KUWAHI KUTOKEA HAPA DUNIANI.Robert wadlow

Si jambo la kawaida hata kidogo ,haliumizi moyo ila ni jambo la kustaajabisha.

Katika moja ya mada ambazo ziligonga vichwa vya habari pande zote kuu za dunia,japokua
najua wengi wetu hatukuwepo.Ni kumuhusu Robert wadlow.
Leo naomba niwarudishe nyuma kidogo miongo kadhaa.
Ilikua ni tarehe 22 February 1918 katika mji wa Alton, Illinois kule nchini marekani ,alizaliwa kijana Robert wadlow akiwa ni mtoto wa kwanza kati ya watoto watano wa familia ya bwana Harold Franklin wadlow na bibi Addie Johnson.
Kijana Robert wadlow alizaliwa akiwa na uzito wa kg 3.8 na kimo chake kikiwa futi 1.8.
Alipofikisha umri wa miaka 8 tu tayari kimo chake kilikua ni zaidi ya baba yake mzazi akiwa na urefu wa futi 6 na uzito wa kg 77.
Robert wadlow akiwa shule walilazimika kumtengenezea dawati lake special, ukirejea katika picha unamuona Robert akiwa amesimama na baba yake mzazi.
Ama kweli ukistaajabu ya MUSSA basi utayaona ya FILAUNI.
Mwaka mmoja kabla ya mauti kumfika 1939 Robert alitajwa kuwa yeye ndiye binadamu mwenye kimo kirefu zaidi kuwahi kutokea katika kizazi hiki na kuingizwa katika kumbukumbu ya kitabu cha maajabu ya dunia al maarufu (WORLD BOOK OF GUINNESS) hivyo akawa ameingia kwenye kumbukumbu hiyo akiwa na urefu wa futi 8.11 na uzito wake ukiwa kg 199.
Mnamo tarehe 15 July 1940 akiwa na umri wa miaka 22 ,miaka mitano baada ya kuingia katika utu uzima alifariki dunia na alizikwa katika makaburi ya oakwood cemetery kule Alton Madison county Illinois katika nchi ya marekan.
Robert wadlow

Robert wadlow


Post a Comment

0 Comments