MICHAEL MTANZANIA

ONESTEPMEDIATZ

Ndemla ashindwa kusaini Mkataba mpya Simba


KIUNGO wa Simba, Said Ndemla, juzi alishindwa kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuichezea Simba baada ya kutofikia makubaliano na uongozi wa klabu hiyo yenye makao makuu yake mtaa wa Msimbazi, Kariakoo jijini Dar es Salaam.


Mkataba wa Ndemla ambaye alianzia katika timu ya vijana ya umri chini ya miaka 20 (Simba B) na mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara ulishamalizika tangu Machi mwaka huu.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zilizopatikana jana zinaeleza kuwa Ndemla aligoma kusaini mkataba mpya na klabu hiyo kutokana na kutoridhika na kiasi cha fedha ambacho walitaka kumpa.

"Ndemla hajasaini, mambo mengine yote yalikuwa sawa kasoro dau la usajili, ila wamepanga kukutana naye tena keshokutwa (kesho)," kilisema chanzo chetu.

Hata hivyo, Ndemla aliliambia gazeti hili kuwa kama atashindwa kukubaliana na Simba, atafanya uamuzi wa kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya nchi.

"Nimeanza mazungumzo na timu yangu na yapo vizuri, muda wowote ninaweza kusaini mkataba mpya, nina ofa nyingi, lakini ninaipa Simba nafasi kubwa, na kama nitaondoka, basi itakuwa ni kujiunga na klabu ya nje ya nchi," alisema kiungo huyo.

Ndemla ni mmoja wa wachezaji wanaotajwa kutakiwa na Yanga na endapo Simba itashindwa kufikia makubaliano naye, huenda akahamia upande huo wa pili.

Post a Comment

0 Comments