KIPUTE cha Kombe la Dunia kinatarajiwa kuanza kesho kwa wenyejiUrusi kuvaana na Saudia Arabia kwenye mchezo unaosubiriwa kwa hamu kubwa.
Urusi ndiyo wenyeji wa michuano hiyo na wanapewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri ingawa timu yao haina wachezaji wenye majina makubwa. Mechi hiyo ambayo itaanza saa 12 jioni kwenye Dimba la Luzhinki, inatarajiwa kuonyesha picha halisi ya michuano hiyo itakavyokuwa.
Kesho kutakuwa na mchezo huo tu, ambapo kwenye asilimia Urusi wanapewa 68 za kushinda, huku Saudia Arabia ambayo nayo haina mastaa ikipewa asilimia 10, sare
ikiwa ni asilimia 22. Hofu kwa mashabiki wa Urusi ni kitendo cha nchi yao hiyo kushindwa kushinda mchezo hata mmoja wa kujiandaa na michuano hiyo ingawa wachambuzi wengi wa soka wanaamini kuwa siyo kipimo sahihi.
Timu hiyo iliyopo chini ya kocha Stanislav Cherchesov, ipo Kundi A na Misri, Saudia Arabia wenyewe
na Uruguay ambao wanapewa nafasi kubwa ya kuwika kwenye kundi hilo.
Timu hiyo inamtegemea zaidi mshambuliaji wake Denis Cheryshev ambaye anacheza kwenye kikosi cha Villarreal, lakini pia ikiwa na kipa mkongwe Igor Akinfeev ambaye anakipiga CSKA Moscow ya nchini kwao.
0 Comments