Utamu wa Ligi Kuu Bara umefika pazuri na ndiyo pazia la ligi hiyo linaelekea kufungwa kwa msimu wa mwaka 2017/18 huku Simba ikiwa imesaliwa na pointi moja kuweza kutangazwa kuwa bingwa rasmi wa ligi hiyo.
Lakini kwa upande wa timu ambazo zinashuka daraja, bado kumekuwa na vuta nikuvute ambapo wale ambao wanashuka rasmi bado hawajafahamika kutokana na timu takribani nne za chini zikiwa na hali mbaya.
Tukigeukia kwa upande wa wachezaji, ushindani umezidi kuongezeka na huku kila mmoja akionekana kuonyesha ufundi wake.
Baadhi ya wachezaji wameendelea kuonyesha ubora wao msimu huu baada ya kuondoka katika timu ambazo walikuwa wakizitumikia msimu uliopita.
Kuondoka kwao sio tatizo na ili k u o n y e s h a wao ni bora walipokutana na waajiri wao wa zamani waliweza kuwafungua, hiyo ni kwa msimu huu ingawa.
Licha ya kufunga kwao mabao hayo, w a c h e z a j i hao hawakuweza kushangilia huku baadhi yao wakionyesha ishara ya kuomba msamaha.
Wafuatao ni baadhi yao ambao mpaka sasa wamefanikiwa kuzifunga timu zao walizozihama mwanzoni mwa msimu huu na wengine katikati ya msimu.
1.GADIEL MICHAEL – YANGA
Ulikuwa ni mchezo ambao ulipigwa katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar ambapo beki huyo wa kushoto alifanikiwa kufunga bao lake dhidi ya waajiri wake hao wa zamani, lakini kwenye mchezo huo beki huyo hakuweza kushangilia bao hilo.
Katika mchezo huo, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1. Gadiel alijiunga na Yanga mwanzoni mwa msimu huu akitokea Azam FC.
2.MBARAKA YUSUF – AZAM FC
Mshambuliaji huyu msimu uliopita alifanya vyema akiwa na Kagera Sugar kutokana na spidi yake ya ufungaji mabao ambapo alimaliza msimu akiwa na mabao 12.
Msimu huu anaitumikia Azam FC na alipoenda na kikosi chake hicho kipya kucheza dhidi ya timu yake ya zamani ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba, alifunga bao pekee ambalo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo huo ulimalizika kwa Azam kushinda 1-0.
Msimu huu mshambuliaji huyo hana kasi nzuri ya kufunga mabao kwani mpaka sasa amefanikiwa kufunga mabao matatu pekee.
3.ADAM SALAMBA –LIPULI FC
Unaweza kusema alikuwa na wakati mbaya kipindi ambacho alicheza na Stand United ambayo ndiyo timu yake ya kwanza kuitumikia ligi kuu.
Kitendo cha Salamba kufunga bao moja katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Stand katika Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, hakuweza kushangilia bao hilo, lakini mashabiki wa Stand United walimpiga mshambuliaji huyo kwa chupa za maji.
Salamba amejiunga na Lipuli katika usajili wa dirisha dogo akitokea Stand United.
4.RAPHEL DAUD – YANGA
Wakati Yanga inacheza na Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya na timu hizo kutoka sare ya kufungana bao 1-1, kiungo huyo wa zamani wa Mbeya City ndiye aliyeifunga Yanga bao hilo.
R a p h a e l alianza kuifungia Yanga bao kabla ya Mbeya City haijas awazisha dakika za majeruhi. K i u n go huyo amejiunga na Yanga m w an z o n i mwa msimu huu akitokea Mbeya City.
5. MCHA HAMISI –RUVU SHOOTING
Ni mmoja kati ya wachezaji ambao walidumu ndani ya Azam FC kwa muda mrefu na hii ni kutokana na umahiri wake katika safu ya ushambuliaji. Hivi sasa yupo Ruvu na amefunga mabao sita katika ligi.
Lakini Azam ilimuacha msimu uliopita na msimu huu anakipiga ndani ya kikosi cha Maafande wa Ruvu Shooting ambapo akiwa Uwanja wa Mabatini alifanikiwa kuifunga Azam na kwenye mchezo huo Ruvu waliibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Licha ya kwamba Ruvu Shooting ilikuwa ikicheza kwenye uwanja wake wa nyumbani, lakini Mcha hakuweza kushangilia bao hilo na badala yake alinyoosha mikono juu na kuomba msamaha.
CHANZO: CHAMPIONI
0 Comments