Mwanaume mmoja nchini Zimbabwe amekamatwa kwa kujaribu kutaka kumfanyia mtihani wa sekondari mpenzi wake. Mtu huyo alivalia mavazi ya kike na kuweka nywele bandia pamoja na kupaka rangi mdomo ili kufanana na mwanamke.
Kwa mujibu wa mtandao wa Naija.com mwanaume huyo alikamatwa katika chumba cha mtihani alipokuwa akijaribu kufanya mtihani huo
katika shule moja iliyopo nchini Zimbabwe, ambapo wasimamizi wa chumba hicho cha mtihani walimtilia shaka na kuanza kumkagua.
Moja ya wasimamizi hao amesema kuwa mwanaume huyo amefikishwa katika vyombo vya ulinzi kwa mahojiano maalum.
0 Comments