MICHAEL MTANZANIA

ONESTEPMEDIATZ

Sababu 3 kwanini Davido ana mzuka na collabo yake na Joh Makini

Septemba 18, 2015, kwa mara ya kwanza Davido alitweet kueleza ujio wa collabo yake na Joh Makini.

April 3, 2017, Davido pia alipost picha Instagram inayoonesha kuwa wawili hao wameshoot video ya collabo yao.

Kwa kila namna, inaonesha kuwa Davido anaikubali sana ngoma hii aliyoshirikishwa na Mwamba wa Kaskizini kiasi cha mara zote kuwa wa kwanza kutoa updates. Hizo, ni dalili njema kuwa wimbo huu utakuwa mkubwa Afrika. Hii inakuwa collabo yake ya
pili kushirikishwa na msanii toka Afrika Mashariki baada ya Number One ya Diamond. Swali ni, kwanini staa huyo wa Nigeria ameonesha kuwa na mzuka sana na project hii? Nimekuandalia ‘theory’ hizi tatu:

1. Davido ni shabiki mkubwa wa Joh Makini

Kabla ya hata kutweet kuhusu collabo yao, Davido aliwahi kusema wazi kuupenda wimbo Nusu Nusu wa Joh Makini. Ni wazi kuwa amekuwa akipenda ngoma za Joh kwa muda na ndio maana ilikuwa rahisi kuirukia ngoma ya Joh.

2. Davido anajua anavyokubalika Tanzania (Afrika Mashariki)

Tangu ashirikishwe na Diamond kwenye Number One, Tanzania imekuwa katika mahali special moyoni mwa Davido. Pamoja na kwamba kuliwahi kutokea uhasama kati yake na mashabiki wa muziki Bongo kutokana na kauli yake ya ‘And they steal again’ baada ya Idris Sultan kushinda shindano la Big Brother Africa, yote yalipita na upendo ukarudi sehemu yake. Hadi sasa Davido ni jina lenye uzito mkubwa Bongo na pia idadi kubwa ya followers wake kwenye mitandao ya kijamii hasa Instagram, ukitoa Nigeria, ipo Tanzania

3. Ngoma ni kali


Mimi nimepata bahati ya kuisikia ngoma hii. Naelewa kwanini Davido ameipania, ni kali sana. Naamini itamfikisha Joh Makini kwenye level za juu zaidi Afrika

Post a Comment

0 Comments