MICHAEL MTANZANIA

ONESTEPMEDIATZ

Mashambulizi ya kemikali yaua 100 Syria

Image result for milipuko syria
Watu wapatao 100 ikiwa ni pamoja na watoto 25 wameuawa nchini Syria kufuatia mashambulizi ya kemikali katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi.
Mashambulizi hayo ya eneo la kaskazini-magharibi mwa Syria yametumia gesi ya sumu iliyopelekea baadhi ya watu kubanwa na pumzi, kutapika, na wengine kutokwa na mapovu midomoni, kulingana na maelezo ya Rami AbdelRahman wa Shirika la Uangalizi wa Haki za Binaadamu la Syria lenye makao yake Uingereza. Mashambulizi hayo yametokea eneo la Khan Sheikhoun katika jimbo la Idlib.

Mjini New York Umoja wa Mataifa imelaani mashambulizi hayo, na msemaji mkuu wa umoja huo Stephane Dujjaric amewaambia waandishi habari kuwa ripoti za aina yoyote za matumizi ya silaha za kemikali, hasa dhidi ya raia ni za kutisha sana. Amesema matumizi ya silaha za kemikali popote ni tishio kwa amani na usalama wa kimataifa na ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa.

Post a Comment

0 Comments