MICHAEL MTANZANIA

ONESTEPMEDIATZ

Kiungo wa Yanga Niyonzima: ‘Haina haja ya kupeleka mechi Mwanza, maandalizi ndio kila kitu’

Kiungo wa Yanga raia wa Rwanda Haruna Niyonzima ambaye pia ni nahodha msaidizi wa timu hiyo amesema, katika soka la kisasa maandalizi ndio kilakitu katika kuhakikisha timu inapata matokeo na sio kubadili uwanja.

Hivi karibuni Yanga iliwasilisha maombi shirikisho la soka Afrika CAF ili mechi yao ya nyumbani ya mchujo kutafuta nafasi ya kucheza hatua ya makundi ya kombe ka shirikisho barani Afrika ichezwe kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mwanza badala ya uwanja wa taifa. Maombi hayo hayakufanikiwa baada ya uwanja wa CCM Kirumba kutokidhi viwango vya CAF na kutakiwa kufanyiwa marekebisho ambayo hayawezi kukamilika ndani ya muda kabla ya mechi hiyo.

“Ukijiandaa vizuri haijalishi uwanja, Mwanza sio mbali mashabiki wanasafiri hadi nje ya nchi sasa Mwanza watashindwaje kwenda kwa hiyo presha ambayo tunaipata hapa haitakuwa tofauti sana na ya Mwanza kwa sababu ni Tanzania ileile.”

“Kwa upande wangu haina haja kubadili uwanja kwa sababu mpira unaweza kuchezeka sehemu yoyote. Sidhani hata kama walimu walipendekeza hivyo, itakuwa ni wadau lakini mpira wa kisasa hauko hivyo, sehemu yoyote unacheza mpira inategemea na wewe ulivyojiandaa.”

Kwa maana hiyo, Yanga itacheza mechi yake dhidi ya MC Algers kwenye uwanja wa taifa Dar es Salaam na si vinginevyo.

Post a Comment

0 Comments