Tunda Man adai kuna wasanii ‘feki’ wanapewa promo kubwa kuliko wasanii wuwezo
Msanii mkongwe wa muziki kutoka Tip Top Connection Tunda Man amedai kuna wasanii wengi hawajui muziki lakini wanabebwa na baadhi ya madj pamoja na watangazaji.
Muimbaji huyo amedai hali hiyo imesababisha baadhi ya wasanii wengi wenye uwezo kuendelea kusugua benchi wakati wasio na uwezo wakifanya vizuri.
“Kama wewe unasikiliza redio au runinga kuna ngoma utakuta zinapigwa sana na hazina hadhi hiyo ya kupigwa sana ila kwa sababu Dj ni mshikaji wake asipopiga mshikaji wake atakasirika. Kwa hiyo ushkaji ndo unasababisha hayo yote, kwa hiyo kubekana kupo sana ndiyo maana una kuta kuna wasanii wanafanya ngoma kali lakini ngoma zao hazifiki kokote,” alisema Tunda.
Aliongeza,”Mimi siwezi kuwataja lakini wananchi wenyewe wanawajua hao wasanii, kama unaweza kuwahoji wananchi wanaweza kukueleza wasanii hao, ni wengi kwa sababu wasanii wenye uwezo hawapewi nafasi lakini wale wasanii feki ndio ambao wanapewa promo ya kweli,”
Muimbaji huyo amedai hali hiyo inasababisha wasanii wengi wenye vipaji kukata tamaa kwa kwa sababu hawapati kile ambacho wanahitaji
0 Comments