Klabu ya soka ya Yanga itacheza Jumamosi hii mchezo wake wa marudiano wa klabu bingwa ya Afrika wakiwa ugenini dhidi ya Zanaco FC ya Zambia bila washambuliaji wake hatari Amisi Tambwe na Donald Ngoma.
Washambuliaji hao ni majeruhi huku Ngoma akitangazwa kukaa nje ya uwanja kwa msimu huu wote. Wachezaji wengine walioshindwa kusafiri na timu hiyo kutokana na majeruhi ni pamoja na kipa Beno Kakolanya, Pato Ngonyani, Yussuf Mhilu, Malimi Busungu na Matheo Anthony.
Akiongea na mtandao wa habari za michezo wa Shaffihdauda, Katibu mkuu wa timu hiyo Boniface Mkwasa amesema wachezaji 20 wamesafiri na timu hiyo akiwemo Deogratius Munishi (Dida), Ally Mustafa (Barthez), Oscar Joshua, Mwinyi Haji, Hassan Kessy, Juma Abdul, Vincent Bossou, Andrew Vincent (Dante), Kevin Yondan na Nadir Haroub (Cannavaro).
Wengine ni Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzima, Deus Kaseke, Justine Zulu, Said Juma (Makapu), Juma Mahadhi, Simon Msuva, Geoffrey Mwashiuya, Obrey Chirwa na Emanuel Martin. Katika mchezo wa kwanza Yanga ilitoka sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Zanaco katika uwanja wa taifa uliopo jijini Dar es Salaam.
0 Comments