MICHAEL MTANZANIA

ONESTEPMEDIATZ

Serengeti Boys imepata ushindi kwa Burundi

Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ imepata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Burundi kwenye mechi ya kirafiki ya kimataifa iyochezwa kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera.


Mechi hiyo ni mfululizo wa maandalizi ya Serengeti Boys ya kwenda kushiriki michuano ya AFCON  kwa vijana chini ya miaka 17 inayotarajia kuanza mwezi May mwaka huu.

Magoli ya Serengeti Boys yamefungwa na Muhsini Makame dakika ya 20 kipindi cha kwanza huku goli la pili likifungwa na Nickson Kibabage dakika ya 38 kabla ya Yohana Mkomola kufunga bao la tatu kwa mkwaju wa penati dakika ya 72 baada ya beki wa Burundi kuunawa mpira ndani ya 18.

Serengeti Boys itarudiana tena na Burundi kwenye mechi ya kirafiki April 1, 2017 halafu itarejea Dar kucheza na Ghana mechi ya kirafiki kabla ya kuelekea Morocco kuweka kambi ya maandalizi kwa ajili ya kwenda Gabon kwenye michuano ya AFCON kwa vijana wa U17.

Post a Comment

0 Comments