MICHAEL MTANZANIA

ONESTEPMEDIATZ

Ramadhani singano awika dhidi ya bambane kombe la shirikisho



Wawakilishi wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho, Azam FC wameanza vizuri michuano hiyo kwa kuichapa Mbabane Swallows ya Swaziland kwa bao 1-0.

Mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, leo ilihudhuriwa na mashabiki wengi waliotaka kuona Azam FC inamaliza kazi mapema.

Hata hivyo, Azam FC ililazimika kusubiri kwenye robo ya nne ya dakika 90, yaani dakika 25 za mwisho kupata bao dhidi ya Mbabane ambao walikomaa hadi mwisho wa dakika 45 mambo yakiwa 0-0.


Hata hivyo, ushindi huo unailazimu Azam FC kuwa makini zaidi kulinda ushindi wake huo mfinyu itakapokuwa ugenini mjini Mbabane katika mechi ya pili itakayoamua matokeo.

Azam FC walipoteza nafasi kadhaa za wazi ambazo zingewawezesha kupata ushindi, lakini hawakuwa wazuri katika suala la umaliziaji.

Dakika za mwanzo, wao ndiyo waliotawala mchezo kwa kiasi kikubwa lakini kadiri muda unavyosonga mbele, wageni wakaanza kuzoea na kuonyesha mchezo wao mzuri.

Post a Comment

0 Comments