Waziri wa Mpya wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe ameanza kazi katika Wizara mpya.
Lakini Dk Mwakyembe ambaye kitaalamu ni
mwandishi wa habari na mwanasheria nguli, amesema hapendi kuona timu za Tanzania zinafungwafunwa tu.
"Watanzania
tumechoka na huu uteja, kusukumwa sukumwa tu kwenye soka. Ni hamu ya
watanzania sasa tuonekane katika ulimwengu wa soka", amesema Waziri Dk.
Mwakyembe aliyezungumza na Kamati ya Hamasa kwa Serengeti Boys
alipokutana nayo kwa mara ya kwanza jana Machi 25, mwaka huu.
Waziri alikwenda mbali kwa kuiagiza Wizara yake yote ijikite kuhakikisha maandalizi ya Serengeti Boys yanakamilika kwa wakati.
"Nataka Wizara yangu yote sasa wimbo wetu uwe Serengeti Boys," amesema Dk. Mwakyembe.
Katika
hafla hiyo, Dk Mwakyembe amempongeza mtangulizi wake, Mheshimiwa Nape
Nnauye kwa kuunda Kamati ya Serengeti Boys ili kutoa hamasa ya
Watanzania kwa timu yao.
Alisema Serengeti Boys ni nyota wanaoinukia (upcoming stars) na wanampa sababu ya kuanza kwenda mpirani tena.
Waziri
Dk Mwakyembe aliendelea kusema kuwa michezo ya leo inahitaji uwekezaji
hivyo Wizara yake itahakikisha kuwa jukumu hilo analibeba.
"Naona
kama imechelewa, lakini bado muda upo, tukimbie, nataka Wizara nzima
wimbo wetu uwe Serengeti Boys", alisema kwa hamasa kubwa.
Dk
Mwakyembe amempongeza Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Mwenyekiti wa
Kamati ya Serengeti Boys, Charles Hilary kwa mafanikio ya program ya
mageuzi ya soka nchini.
Naye
Mkurugenzi wa Michezo katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Yussuf Singo alisema sasa imechoka kuwa kichwa cha mwenda
wazimu na hivyo Taifa limeazimia kucheza Kombe la Dunia kupitia vijana
wa Serengeti Boys.
Rais
wa Shirikisho la Kandanda Tanzania, Jamal Malinzi alisema kufuzu kwa
Serengeti Boys kucheza fainali za AFCON ni sifa pekee na mwanzo mpya wa
mageuzi makubwa ya soka la Tanzania.
Amesema maandalizi ya ushiriki wa fainali za AFCON zitahitaji takriban Shilingi bilioni moja.
Amesema mikakati mbalimbali imeandaliwa kuchangisha kiasi hicho cha fedha, ikiwa ni pamoja na kuandaa chakula cha hisani.
Waziri Mwakyembe amesema atahakikisha fedha hiyo inapatikana ili vijana wa Serengeti Boys waweze kufuzu kucheza kombe la dunia huko India mwishoni mwa mwaka huu.
Waziri Mwakyembe amesema atahakikisha fedha hiyo inapatikana ili vijana wa Serengeti Boys waweze kufuzu kucheza kombe la dunia huko India mwishoni mwa mwaka huu.
0 Comments