MICHAEL MTANZANIA

ONESTEPMEDIATZ

: Mdogo wake Gwajima alizungumzia sakata dawa za kulevya, ampinga kaka yake

Mdogo wake na mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la ufufuo na uzima, Methusela Gwajima amesema mchungaji huyo anatakiwa aache kutumika na kuhoji kuna nani nyuma yake.



  
   .             .          .     .        Mdogo wake Gwajima, Methusela Gwajima

 Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika katika holeli ya Traveltime Kinondoni jijini Dar es salaam, Methusema amedai mchungaji hawezi kujiingiza kwenye malumbano na mipasho ya kidunia.

“Katika hilo watanzania naomba sana tumpuuze, nasema tumpuuze kwa sababu hoja zake zimejikita katika lengo la kutafuta defance, kutafuta kinga.

Umeshatuhumiwa, umeitwa polisi, kwa nini usisubiri uchunguzwe, wameitwa watu wengi wameenza kwanini yeye analifanya hilo jambo kuwa ajenda, mbaya zaidi imekuwa ni ajenda kanisani, kwahiyo kanisa limegeuzwa kuwa kijiwe cha siasa lakini watanzania wamekaa kimya hawasemi,” alisema Methusema.

Ameendelea kusema vyeti vya Makonda viachiwe mamlaka husika kuchunguza kwani kumuandama sana inaweza kusababisha watu wengine siku zijazo kuogopa kujihusisha kupambana na madawa ya kulevya.

Amesema serikali imemlea sana Gwajima na waziri wa mambo ya ndani anatakiwa amuangalie na ana tuhuma nyingi ikiwemo kadai angemfufua baba wa watoto yatima ilhali yeye anajua hajawahi kufufua hata panya.

Amedai tabia ya kubeza shughuli za maendeleo zinazofanywa na serikali sio tabia njema na haiisadii nchi. Amesema anajua vita ya madawa ya kulevya ni ngumu na hugharimu maisha, atoa wito kwa watanzania wote kuunga mkoni juhudi za kutokomeza madawa ya kulevya hasa Dar es Salaam.

Amesema anafahamu yeyote atakayejitokeza kuunga mkono juhudi za kupambana na madawa ya kulevya ataandamwa tu na hivyo kwa namna ya pekee anamshukuru mkuu wa mkoa wa Dar Paulo Makonda na atakumbukwa na vizazi vyote kwa kujitoa Muhanga kusimamia vita ya madawa ya kulevya Dar es Salaam na kila mmoja amefahamu athari za madawa ya kulevya hadi kwa watoto wadogo ndio maana anaandamwa kila kona na kuhoji walikuwa wapi kuyasema yote kabla ya vita ya madawa ya kulevya.

Post a Comment

1 Comments

Ni sahii jamaa kusema haya ama sio sahii