MICHAEL MTANZANIA

ONESTEPMEDIATZ

Ivan Rakitic akubali kubaki Camp Nou

Mchezaji wa klabu ya FC Barcelona na timu ya taifa ya Croatia, Ivan Rakitic amekubali kusaini mkataba mpya na klabu yake hiyo ya Hispania, ambao utamuwezesha kuwepo Camp Nou hadi
mwaka 2021.

Rakitic amekamilisha mpango huo, baada ya kuhusishwa na taarifa za muda mrefu za kutaka kusajiliwa na klabu za nchini England, na ilifikia hatua ada yake ya usajili ilitajwa kufikia zaidi ya Pauni milioni 100.

Klabu za mjini Manchester zilihusishwa katika taarifa za kumuwania mchezaji huyo mwishoni mwa msimu huu.

Taarifa rasmi zilizotolewa na FC Barcelona zimeeleza kuwa, tukio la kusaini mkataba mpya kwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28, litafanyika wki hii mjini Barcelona.

Rakitic ambaye alisajiliwa na FC Barcelona mwaka 2014 akitokea Sevilla CF, na tayari ameshaitumikia klabu hiyo michezo 145 na amefunga mabao 23.

Post a Comment

0 Comments