MICHAEL MTANZANIA

ONESTEPMEDIATZ

Hivi Ndivyo Samatta Anavyozidi Kuingia Katika Mioyo ya Wazungu Taratibu....!!!


Baada ya kufunga magoli mawili katika michuano ya Europa League dhidi ya ndugu zao KAA Gent Mshambuliaji na Nahodha wa Tanzania Mbwana Samatta huku KRC Genk wakishinda jumla ya magoli 5-2 na kuandikwa na vyombo mbalimbali barani Ulaya hatimaye jana ameifungia timu yake bao katika ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya KVC Westerlo kwenye dimba la Het Kuipje.

Ilichukua dakika ya 7 Mbwana Samatta akifunga goli la uongozi katika timu yake na mnamo dakika ya 27,Thomas Buffel hadi mapumziko wageni walikuwa mbele kwa 2-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote mbili kufanya mabadiliko hata hivyo wageni waliweza kunufaika kwani kunako dakika ya Omar Colley alifunga dakika ya 62 na dakika ya 90,Malinovsky akipingilia msumari wa nne ukiwa mchezo wa kufunga Ligi kuu ya Ubelgiji huku Genk wakifikisha jumla ya pointi 48 kwenye nafasi ya nne ya Msimamo.

Hadi mwamuzi akipuliza kipyenga cha mwisho Genk wameibuka na ushindi wa jumla ya magoli 4-0 huku Samatta akifikisha jumla ya magoli 10.

Post a Comment

0 Comments