MICHAEL MTANZANIA

ONESTEPMEDIATZ

Hawa ni wasanii wa kike wa Bongo Jay Moe anawakubali + rappers wa anaoamini wana uwezo wa kuwakalisha wakongwe

Jay Moe amewataja Vanessa Mdee, Lady Jaydee na Aika wa Navy Kenzo kuwa ndio wasanii wa kike anaowakubali zaidi kwa sasa na ambao angependa kuja kuwashirikisha siku moja kwenye kazi zake.

“Hao ni katika wachache ambao naona wanaipeperusha bendera yetu ya Tanzania,” alisema Jay Moe kwenye mahojiano na kipindi cha Twenzetu cha Times FM.

“Watu kama akina Dayna Nyange pia natamani nifanye nao sababu nakubali anachofanya sababu niliona tangu anaanza mpaka leo alipofikia kwahiyo niko proud pia ikitokea kufanya kazi na mtu kama huyo,” alieleza rapper huyo.


Kwa upande mwingine Jay Moe alitaja baadhi ya rappers ambao anaamini wana uwezo mkubwa kuzidi wakongwe kibao.

“Nakutana nao, kuna wimbo mimi natakiwa nifanye na One The Incredible,” anasema. “One ni kati ya vijana ambao wamekuja zama za sasa hivi ambaye inaniuma ninavyoona hawi kama vile mimi ninataka awe kwasababu uwezo wake ni mkubwa sana hata ukifananisha na wasanii nilioanza nao mimi zama zangu, kuna wengine kibao ambao kiukweli kwa ushairi na nini hawamwezi. Napenda kwasababu anaweza kufanya kwa Kiswahili vizuri, kwa Kiingereza vile vizuri na ukiacha hivyo, unampenda mtu pia kutokana na tabia yake na anavyokurespect. Ndio maana hata kwenye interview nyingi nakuwa nataja mtu kama Bill Nass kutokana na respect yake na ile passion yake aliyokuwa nayo kwenye muziki. One the Incredible ni mmoja wapo ambao nawish kesho nimuone akiwa kwenye nafasi ya juu kabisa,” alifafanua Jay Moe.

“Songa, napenda anachokifanya, napenda anavyousoma mchezo, tulimuona Songa wa kabla ya Mwendo Tu na wa kwenye Mwendo tu, unaweza kuona kabisa huyu jamaa akifanya Mwendo tu tatu nne atakuwa yuko mbali. Napenda pia hiyo passion ya hip hop na presentation ambayo wanafanya watu wengine, Wakazi bado anafanya vizuri kwenye ile side ambayo watu wanataka ile hardcore hip hop na ile rap ambao kuna ushairi, silabi na nomino za kutosha Nikki Mbishi bado yupo kwenye hiyo nafasi pia.”

Post a Comment

0 Comments