Kumiliki mjengo kwa Dar sio mchezo mchezo lakini Harmorapa ni baba mwenye nyumba pia kwa sasa, walau kutokana na maneno yake mwenyewe.
Rapper huyo machachari amethibitisha kuwa kwa sasa anamiliki nyumba ambayo ipo maeneo ya Mikocheni jijini Dar es Salaam aliyonunuliwa na uongozi wake unaomsimamia.
“Yaah nimenunuliwa nyumba maeneo ya Mikocheni na bosi wangu Irene Sabuka. Nyumba hiyo ipo fresh ina vyumba viwili na sitting room na bafu na kila kitu ambacho staa anastahili kumiliki. Menejimenti imeamua kufanya hivi ili niweze kuwa kwenye nyumba ya hadhi ya staa kama mimi,” Harmo amekiambia kipindi cha Kubamba cha Times FM.
Kwa sasa rapper huyo anatamba na wimbo wake wa ‘Kiboko ya Mabishoo’ ambao amemshirikisha Juma Nature huku ndani yake akiwa amewaponda baadhi ya watu akiwemo Mose Iyobo na wengine.
0 Comments