Harry Kane, moja ya washambuliaji bora kabisa duniani akiwa na umri wa miaka 24. Muingereza huyu anasifika kwa kutikisa nyavu akiwa uwanjani amechezea Tottenham, michezo 149, na kufunga mabao 109, katika michezo ya ligi kuu Uingereza. ana ufanisi mkubwa mno wa kufunga.
Akiwa uwanjani ni mkimya mno sana baadhi ya mabeki huwa wanapata tabu kumkabili.
Raisi wa klabu ya Real Madrid, Fiorentina Perez, anamtolea macho na kumtaka ajiunge na miamba hiyo ya nchini Spain.
Umri wa Cristiano Ronaldo haujabakiza chenchi, unazidi kusonga mbele. Nguvu zake zinaelekea ukngoni na muda sio mrefu atatumbukia shimoni. jua litazama.
Wala tusiogope kusema hakuna mwenye hadhi ya kuvaa viatu vya Ronaldo sababu wengi wananuka miguu. Ni Hary Kane ndiye mwenye uthubutu huo kwa kiwango cha ufungaji alichonesha
Msimu wa mwaka 2015/16, alibuka kinara wa mabao katika ligi kuu Uingereza, akifunga mabao 25, na kutwa kiatu cha dhahabu msimu huo katika ligi kuu. Tottenham walimaliza nafasi ya 3 , wakiwa na alama 70.
Kuna utofauti mkubwa kati ya Harry, na timu anayochezea. Ni kama Masikini aliokota milioni
Msimu wa mwaka 2016/17, Muingereza, huyo alibuka tena mfungaji bora wa ligi kuu England, akiwa amefunga mabao 29, huku Tottenham, wakimaliza nafasi ya 2, kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 86. Katika misimu yote msimu huo ndo walivuna alama nyingi zaidi Tottenham.
Huyo ndio Kane na ubavu wake. Yupo Kane anayebeba miili ha akina Great Khali na kuna Kane anayebeba mzigo wa Tottenham.
Msimu huu wa mwaka 2017/18, amemaliza nafasi ya pili nyuma ya mfungaji bora Mohamed Salah, Harry Kane, amefunga mabao 30, tayari kwenye ligi kuu Uingereza. wamemaliza nafasi ya 3, wakiwa na alama 77. Mara ya tatu mfululizo wanakwenda UEFA.
Pia amefunga mabao 30, kwa mara ya kwanza katika ligi kuu Uingereza, ndani ya msimu mmoja tangu alivofanya ivo Kevin Phillips msimu wa mwaka 1999/2000.
Mwenyekiti wa klabu ya Tottenham, Daniel Levy, amesema kuwa kama kuna timu inamuhitaji mchezaji huyu waje na paundi million 200. Sawa Je hii si ni hela ha maandazi kwa dunia ya sasa?
Tottenham washampiga pingu mchezaji huyo huku wakiamini Real hawawezi kumpata.
Mwenyekiti huyo amekuwa mgumu kuuza wachezaji wake huku akitegemea mtu aje na pesa nzuri ndo maongezi yaanze. Alimuua Gareth bale msimu wa mwaka 2013/14, kwenda Real madrid kwa kitita cha paundi million 85, kisha Luka Modric kwenda Real Madrid kwa kitita cha paundi million 45.
Msimu huu kamuuza kyle walker kwenda Manchester city kwa kitita cha paundi milion 50, jinsi gani anajua kutengeneza fedha. Sasa Kama Bosi wake Kane anajua kutengeneza hela kwanini yeye ashindwe kutengeneza mazingira ya kwenda Madrid ili kupata jela na mafanikio?
Ametuonesha kuwa Harry, anaweza kucheza la liga, kutokana na ubora wake wa kufunga huwa ajali timu imepata matokeo gani yeye anafunga tu.
Watu wengi wanaamini kuwa ligi kuu Uingereza, inaushindani zaidi sawa lakini huo ushindani haumsaidii chochote Kane. Huu ndo muda wa Harry, kuondoka na kwenda kutafuta mafanikio na aache kumbukumbuku katika soka, tuzo anazo beba ni zake binafsi ,anahitaji mafanikio ya makombe zaidi
0 Comments